20 washikiliwa vuruguza daladala Arusha

Kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
Watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya fujo na kuharibu mali za watu katika tukio la mgomo wa mabasi ya abiria (daladala) juzi.

 
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alisema watu hao wameshikiliwa kutokana na kujihusisha na vurugu hizo na uharibifu wa mali ikiwamo kuvunja vioo vya gari aina ya Toyota Hiece namba za T 171 BE, mali ya Edward Clegori.
 
Alisema pia jeshi hilo linashikilia gari moja aina ya Nissan Caravan namba T 499 CFV, mali ya Gabriel Thomas Malya ambalo lilikuwa linatumika kusambaza vijana waliokuwa  wanafanya fujo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha pamoja na
kuzuia magari mengine kufanya kazi.
 
Baadhi ya wanaoshikiliwa ni Aizaki Wilfred (23), Shaibu Khalifani (20), Gabrieli Thomas (27),  Amani Samosoni, Said Khalifan Juma (19) na Roberty Maico Kamugisha (30) 
 
Alibainisha kuwa watu hao wako mikononi mwa polisi na watafikishwa kortini upelelezi itakapokamilika.

Comments