ROSE MUHANDO KUACHIA NGOMA MPYA SIKU YA PASAKA

Nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando
Nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando atatambulisha albamu yake mpya iitwayo 'Tazama Mungu Anacheka' wakati atakapotumbuiza katika Tamasha la Pasakalitakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.

 
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo amemuhakikishia kuwa amewaandalia mashabiki wake vitu vikubwa kwenye tamasha hilo.
 
Msama alizitaja nyimbo zilizomo katika albamu hiyo kuwa ni 'Mungu Anacheka', 'Tenda Wema', 'Mungu Unishangaza', 'Mwanamke Mbaya', 'Sema Nami', 'Penye Raha', 'Heri Wenye Moyo', 'Shujaa wa Msalaba' na 'Tembea Baba'.
 
Akizungumzia maandalizi ya onesho hilo, Msama alisema yanaenda vizuri na kwamba wasanii wa nje ya nchi wanatarajiwa kuanza kuwasili Alhamisi na kuwaomba mashabiki wakae mkao wa kula kupata mambo mazuri.
 
Wasanii wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza ni kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda ambalo pia linatarajia kuzindua albamu yao mpya iitwayo 'Kaeni Macho'. Nyota wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.
 
Wasanii wa Tanzania waliothibitisha pamoja na Rose Muhando ni Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival, Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro na kundi la Glorious Celebration.
 
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 litakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata litakuwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanz

Comments