MUME WA MTU NUSURA AUAWE NA KAHABA BAADA YA KUGOMA KUMPA MALIPO YAKE

WAKATI Oparesheni Fichua Maovu katika jamii inayoendeshwa na Global   ikiwa kazini, wikiendi iliyopita ilinasa timbwili zito la aina yake kwa mwaka 2013 ambapo mume wa mtu, Joseph Hussein (31), nusura auawe na kimada...
Hatoki mtu hapa: Joseph Hussein akiburuzana na kimada wake Neema Samson baada ya kudaiwa kupenda vya bure.
Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge, Dar mishale ya saa 10 usiku ambapo mwanaume huyo, mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Neema Samson, mkazi wa Buguruni.



  Lazima unipe changu: Neema Samson akiwa amemkaba mteja wake baada ya kushindwa kumlipa chake.
Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama wanavyokubaliana.


“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa hasira.

Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu yake aina ya Nokia.

MJUMBE ATEMA CHECHE
Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti, alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema.

  Baada ya wananchi kuona wapenzi hao wanazidi kuvuruga amani mtaani kwao, waliamua kuwaweka mtu kati tayari kuwapeleka sehemu husika.
SOO HILOOO POLISI
Wawili hao waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema waliposhirikiana kuwabeba kisha kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo cha polisi....

Safari kuelekea kituo cha polisi: Wananchi wakiwabeba msobemsobe kuwapandisha kwenye Bajaj tayari kuelekea kituo cha polisi.

Comments