TAPELI ANAYETUMIA JINA LA MUHESHIMIWA WAZIRI LUKUVI HAPA IRINGA ANASWA KWENYE HARAMBEE YA OVERCOMERS MBELE YA MGENI RASMI MH.LOWASSA

maofisa  wa  polisi mkoa wa  Iringa  wakiweka mtego nje ya  ukumbi wa St Dominic  ili kumnasa  tapeli  huyo anayejiita ni mtoto  wa  waziri Lukuvi  na kutapeli  watu.

 





Tapeli  anayetapeli  watu maeneo mbali mbali ya Tanzania  kupitia jina la  waziri Lukuvi akiingizwa ktk  gari maalum leo
Tapeli  Jonathan Wiliam Lukuvi feki akitiwa matatani askari kanzu  Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dkt  Christina  Ishengoma ,askofu Dkt  Boaz Sollo na Waziri mkuu wa  zamani Edward  Lowassa akimsikiliza tapeli huyo akimpa maneno ya kitapeli  Lowassa
Kijana  huyo Tapeli akimsomesha  waziri Lowassa ukumbini kwa kuahidi kuchangia 100,000 huku akimwomba  kumsaidia misaada  zaidi
Hapa akipelekwa  katika gari maalum Hapa akiingizwa katika Taxi tayari  kwenda  polisi
Kijana ambae amekuwa akiwaliza  watumishi mbali mbali wa umma na watu  binafsi  kwa  kutumia jina la waziri wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu  wa bunge kijana Jonathan Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)amekamatwa katika hafla ya kanisa la Overcomers FM akitaka  kumtapeli  waziri mkuu  wa zamani  Edward Lowassa kupitia harambee  hiyo.
Kijana  huyo  aliingia katika ukumbi  wa  St.DOminic leo  katika harambee ambayo mgeni  rasmi  alikuwa ni Lowassa na  kupita mbele na kutumia kipaza  sauti  kuzungumza kuwa anaitwa  JOnathan Wiliam Lukuvi  na ni mtoto  wa  waziri wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu sera na uratibu  wa bunge na kuwa amekuwa akimpigia  simu mara kwa mara  Lowassa na hata katika mkutano  wake  wa Jangwani  jijini Dar es Salaam alipata  kuzungumza na Lowassa na  hivyo kuomba  kutekelezewa  ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na  utambulisho  huo  baadhi ya  watu  waliopata  kutapeliwa na kijana  huyo akiwemo mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  waliweza kuguna hali iliyopelekea  askari  polisi  kufunguka na kumtia mbaroni  kijana  huyo ambae alikuwa akiweka mtego  wa kumtapeli  Lowassa  na  viongozi  wengine katika hafla  hiyo .
Hata  hivyo  baada ya  polisi  kumtia nguvuni kijana  huyo  baadhi ya  watu  waliotapeliwa  waliweza  kumtambua  huku familia ya  Lukuvi iliyokuwemo katika ukumbi  huo  ikimkana katu katu kuwa hana hata  chembe ya familia na  watu hawamtambui .
Kada  wa CCM maarufu mkoani Iringa Godfrey  Malenga  Lukuvi  alisema   kuwa  kijana  huyo  amekuwa akitumia  jina la waziri Lukuvi  kuliza  watu na kuwa wengi  wamekuwa  wakilalamika  kuhusu  utapeli  unaofanywa na kijana  huyo na kuwa tayari alipata kukamatwa na  polisi ila alitolewa .

Kwa  upande  wake  katibu  wa mbunge  jimbo la Isimani ambae  pia ni familia ya  Lukuvi Bw  Thom Malenga  Lukuvi alisema  kuwa amekuwa akipokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali ambao  wamelizwa na kijana  huyo na kuwa  siku  zote  alikuwa akiweka mtego ili kumnasa kijana  huyo tapeli  japo hakufanikiwa  kumpata.

Thom ambae  yupo  nje ya mkoa  wa Iringa  kwa shughuli za kifamilia  alisema kuwa alitamani  sana kama angebahatika  kumshuhudia kwa macho kijana  huyo tapeli  ila kwa kuwa  yupo nje ya mkoa atajitahidi  kurudi mapema mjini Iringa ili kumwona  tapeli huyo.

Kwa  upande  wake mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  Teresia Mahongo alimweleza mwandishi  wa mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com kuwa pia kijana  huyo alipata  kufika  ofisini kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya  kumshtukia alimtafuta  waziri Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa  kijana  huyo ni tapeli  mkubwa .

Hata  hivyo  mwanahabari  Gerald Malekela  wa radio  Nuru  Fm alisema kuwa  kijana  huyo alipata  kufika  studio  za radio  hiyo kwa ajili ya  kutapeli  uongozi kwa  kutumia jina  hilo na kufika  studi  za radio hiyo huku akiwa na barua inayosifia  watangazaji na kuomba  kusaidiwa  zaidi kama mmoja kati ya  wasikilizaji .
 Mtandao huu ulipata nafasi ya  kumtafuta  kwa  njia ya simu  waziri  Lukuvi ambae  mbali ya  kumkana kuwa hamtambui  bado alisema  kuwa amepata   kuwaliza  watu mbali mbali kwa  kutumia jina lake.

Lukuvi alisema kuwa tayari  amepata kupokea malalamiko kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na kumwagiza  kumtakata na kutaka  sheria  ichukue mkondo  wake.

"Mimi  huyu  kijana  simtambui na  wala  si ndugu yangu ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli  watu na tayari alikamatwa na polisi kwa  utapeli  huo"

Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Dkt  Christina  Ishengoma aliwaonya  watu  wanaoendelea  kutapeli  wengine kwa  kutumia majina ya viongozi ama namna nyingine  yeyote kuacha mara moja na kuwa  akiwa kama mwenyekiti  wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa hatakubali kuona  matapeli hao  wakiendelea  kulizwa  watu kwa njia ya udanganyifu .


Hata  hivyo aliwataka  wananchi  kujiepusha na wimbo  hilo la utapeli kwa kuwaripoti  polisi  watu  wanaowashukia kuwa ni matapeli .

Comments