MASTAR WA BONGO MOVIES WAMTOSA BABA HAJI KATIKA MAHAFALI YA KUHITIMU CHUO CHA SANAA BAGAMOYO


Msanii wa filamu tanzania ambaye ameamua kuwekeza katiaka kusomea filam huko chuo bagamoyo katika chuo cha sanaa Haji Adam Dach amemafanya mahafali yake na kumzungumza na JAMIILEO TZ .BLOGSPOT.COM
Akizungumza na mwandishi wetu baba haji amesema kuwa kwanza anayofuraha kutimiza malengo yake ambayo alikuwa anayaota kila siku na pia anaamini kuwa sasa atafanya kila linalowezekana ili kuleta mabadiliko ya sanaa nchini tanzania.

Muda wote haji alionekana mwenye furaha japo furaha yake ilianza kupotea baada yakona muda una kwenda na wasanii wenzie ambao kwake ni kama ndugu wakiwa wamemtosa na kutokufika kabisa katika sherehe hizo zilizofanyika katika maeneo hayo ya chuo Kaka unajua siamini kabisa kaka yaani hadi sasa naona ndugu zangu wamenitenga na hakuna dalili za kufika kwao maana nimepiga simu nyingi zinaita bila majibu huku nyingine zikiwa zimezimwa kabisa

Mwandishi wa thesuperstarstz alibahatika kukutana na msanii Single mtambalike au Rich Rich na kuongea nae ambae alisema kuwa hata mimi sitaki kuamini kama mastar wameamua kumtosa mwenzao kwani wote wanajua na ilibidi jamba kama hili tuungane kwani haji ameonyesha mfano kwa kwenda kuwekeza katika elimu sasa inanishangaza sijui ni wivu au ni roho mbaya hata sijui mimi imeniuma sana kaka alisema Rich
Wasanii waliowasili katika mahafali hayo ni pamoja na Rich Rich,Natasha na Monalisa jambo lililofanya baadhi ya watu wa chuoni hapo kupigwa na butwaa kwani wanachuo walijipanga kukutana na mastar ambao iliaminika wangeenda kumsapoti super star mwenzao ambaye ametumikia chuoni hapo kwa miaka mitatu sasa.
Baadhi ya wanachuo waliongea na mwandishi wa JAMIILEO TZ.BLOGSPOT,COM nakusema kutopendezwa na tukio lile na kusema hawajamtendea haki ndugu yao ambae amekaa nao katika gemu kwa miaka kumi na mbili sasa lakini wameshindwa kumsapoti,walisema wanachuo hao na kuponda ustaa wa tanzania

Comments