MH. HALIMA MDEE (MBUNGE ) AKIFANYA MAZOEZI YA NGUMI KWA AJILI YA KUMCHAKAZA JACKLINE WOLPER




Mbunge wa Kawe (Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi dhidi ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
Pambano la wakali hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.
Mdee amekuwa akiendelea na mazoezi yake chini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye pia siku hiyo atapanda ulingoni kutoana jasho na mkali wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’


Katika tamasha hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao lililosisimua.
Lakini Mdee ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam.

Comments