MISS UTALII TANZANIA 2013 SASA KUMEKUCHA:SOMA HAPA KUFAHAMU USIYOYAJUA:


  • Baada ya kukuru kakara za mwaka huu za fainali za mikoa, kanda ,Taifa na hatimaye Miss Utalii Morogoro 2013, Hadija Said Juma kuibuka mshindi wa taji la Miss Utalii Tanzania 2013, bodi ya mashindano hayo imeanza kufanya kweli katika kutekeleza ahadi yake ya kupeleka zaidi ya washindi watano katika mashindano ya dunia na mengine ya kimataifa mwaka huu.


    Kishindo cha Miss Tourism Tanzania Organization, kilianza kusikika jana baada ya mshindi wa tano wa Miss Utalii Tanzania 2013, Mwanakombo Mbasha, kuondoka nchini kwa ndege ya shirika la ndege la Turkish Airline kuelekea nchini Kosovo,kupitia Uturuki kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Freedom Of The World 2013.

    Mashindano ya Miss Freedom of The World 2013, yatafanyika tarehe 24 -6-2013, katika hoteli ya kitalii ya T & A Hotel jijini Prizren. Mashindano hayo yanashirikisha zaidi ya nchi 80 duniani kote.

    Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere , Mwanakombo alisindikizwa na washiriki na washindi mbalimbali wa Miss Utalii Tanzania 2013, akiwemo mshindi wa Pili wa Miss Utalii Tanzania 2013,ambaye pia ni Miss Utalii Dar es salaam 2013 Lucy Noel na mshindi wa tuzo ya Taifa ya Mazingira ya Miss Utalii Tanzania 2013 Happy Kikota ambaye pia ni Miss Utalii Arusha 2013.Mrembo huyo anatarajiwa kurejea nchini 30-6-2013, kwa ndege ya shirika hilohilo.

    Aidha Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija saidi Juma, atawakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Tourism world 2013, ambayo yatafanyika nchini Equatorial Guinea 12 Octoba 2013, pia washindi wengine wa tano bora watawakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss International 2013 yatakayo fanyika Japani, Miss Tourism United Nation 2013 yatakayo fanyika Nigeria Disemba 2013, Miss Globe International yatakayo fanyika Uturuki Disemba 2013, Miss University World 2013 na Miss heritage world 2013.

    Akiwa uwanjani hapo, Mwanakombo aliahidi kurudi na Taji katika mashindano hayo na aliwashukuru viongozi wa Miss Tourism Tanzania Organization hasa rais wake Gideon Chipungahelo kwa jitihada binafsi za kuhakikisha anasafiri na kushiriki mashindano hayo japo katika mazingira magumu ya kutokuwa na wadhamini wala wafadhili.
    Nae Lucy Noel , mshindi wa pili Miss Utalii Tanzania 2013, kwa niaba ya warembo na washindi wote wa Miss Utalii Tanzania , alimtaka mwanakombo kukumbuka mafunzo yote waliyo pewa wakiwa kambini, ikiwemo kudumisha nidhamu na kumtaka akumbuke kuwa anaye shiriki kule si yeye bali ni Nchi yetu tukufu ya Tanzania , hivyo akasimame kidete kuhakikisha kuwa Tanzania tunarudi na taji, huku akifuata nyayo za warembo wote wa Miss utalii Tanzania wa miaka ya nyuma ambao wote kwa mika mitano wamerudi na mataji.

    Akizungumza kwa njia ya simu na Mwanakombo Kessy, kutoka mkoani Morogoro , Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi Juma, alielezea kusikitika kwa kushindwa kuwapo uwanja wa ndege kumsindikiza mwenzie kutokana na majukumu ya kimasomo, alimtaka Mwanakombo siku zote akiwa mashindanoni kutambua kuwa yeye ni Balozi wa Tanzania pamoja na utalii, Uwekezaji na utamaduni wake, hivyo anapaswa siku zote kuzingatia na kuonyesha utamduni wa Tanzania bila aibu na wala kuiga utamaduni kutoka kwa wengine.
    Asante,
    Erasto Gideon chipungahelo
    Afisa Mtendaji Mkuu – Miss Utalii Tanzania

Comments