50 CENT KWENDA JELA AU KULIPA FAINI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MAMA WA MTOTO WAKE

Family Photo - Shaniqua, 50Cent na Marques

50 Cent huenda akajita anakwenda jela miaka mitano na kutakiwa kulipa faini ya zaidi ya dola 46000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 74 za Kitanzania, kwa mashtaka matano aliyofunguliwa yanayotokana na tukio alilofanya June 23 la kumpiga bibie Shaniqua Topmkins ambaye ni mama wa mtoto wake.

 Katika tukio hili, 50 Cent mbali na kumpiga Shaniqua, vilevile alifanya uharibifu katika nyumba yake wa mali yenye thamani ya dola 7,100 zaidi ya shilingi milioni 11 za kitanzania, ambapo vitu kama vile furnitures, taa za mezani, TV na vinginevyo vilivunjwavunjwa, na msanii huyu aliondoka eneo la tukio muda mfupi kabla ya Polisi kukufika.

Huyu ni Mtoto wa 50 Cent, Marques anavyoonekana hivi sasa
Kesi ya msanii huyu itaanza kusikilizwa June 22.

Shaniqua na mwanasheria wake

Comments