WABUNGE MASHABIKI WA YANGA WATWAA KOMBE BAADA YA KUWAFUNGA WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA MBELE YA REFA RAIS KIKWETE

.
baada ya kuanzisha mpira akimpa refa filimbi aendelee
TIMU ya Yanga SC ya Wabunge, imetwaa ubingwa wa Tamasha la Matumaini baada ya kuwafunga Wabunge wa Simba kwa penalti 4-3 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii, kufuatia sare ya bila kufungana.


Kipa hodari kwa michomo ya penalti wa timu ya wabunge mashabiki wa Simba SC,Ni Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye leo aligeuzwa shati tu langoni baada ya kutunguliwa penalti zote zilizopigwa na Wabunge mashabiki wa Yanga.
 
Waliofunga penalti za Yanga ni Michael Kadebe, Mark Tanda, Christopher Kabenyele na Said Mtanda, wakati kwa Simba Yona Kilumbi alipaisha ya kwanza, Amos Makala, Adam Malima na Abel Kigula wakafunga zilizofuata na Aziz Abood akakosa ya tano.

Kipa wa Yanga, Hussein Zubeiry Mbunge wa Fuoni Zanzibar alisimama imara leo kulinda lango Yanga na kuokoa michomo mingi ya hatari.

Mechi hiyo ilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliyeanzisha kabla ya kumuachia refa Athumani Kazi aendelee kama anavyoonekana hapo chini
 
Rais Kikwete akianzisha mchezo

Comments