HATIMAYE NDEGE YA ABIRIA YA ANGUKA NCHINI NIGERIA.soms habari kamili hapa

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 20 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos nchini Nigeria
.
Taarifa kamili zilizolipotiwa na BBC swahili zinasema kuwa watu 8 wamefariki.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka na kulipuka.
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani 
nchini humo.

Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.
Mbali na kueleza watu hao nane wamefariki hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.

Comments