20 washikiliwa vuruguza daladala Arusha
Kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alisema watu hao
wameshikiliwa kutokana na kujihusisha na vurugu hizo na uharibifu wa
mali ikiwamo kuvunja vioo vya gari aina ya Toyota Hiece namba za T 171
BE, mali ya Edward Clegori.
Alisema pia jeshi hilo linashikilia gari moja aina ya Nissan
Caravan namba T 499 CFV, mali ya Gabriel Thomas Malya ambalo lilikuwa
linatumika kusambaza vijana waliokuwa wanafanya fujo katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Arusha pamoja na
kuzuia magari mengine kufanya kazi.
Baadhi ya wanaoshikiliwa ni Aizaki Wilfred (23), Shaibu Khalifani
(20), Gabrieli Thomas (27), Amani Samosoni, Said Khalifan Juma (19) na
Roberty Maico Kamugisha (30)
Alibainisha kuwa watu hao wako mikononi mwa polisi na watafikishwa kortini upelelezi itakapokamilika.
Comments
Post a Comment