37 wanaswa kwa wizi wa maji Dar

Mitambo ya maji.
Watu 37 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa maji jijini Dar es Salaam.
Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia operesheni inayofanywa na Kampuni ya Majisafi na Majitaka (Dawasco) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa) inayomiliki miundombinu ya huduma hiyo.
Mamlaka hizo ziliamua kuendesha operesheni hiyo kufuatia kukithiri kwa wizi wa maji na hivyo kuwasababishia wakazi wengi wa Jiji la la Dar es Salaam kukosa huduma hiyo muhimu
.
Wizi huo ni pamoja na ule wa kukwepesha mita, kujiunganishia, kukatisha laini na kusababisha wakazi wa eneo husika kukosa maji huku yakiuzwa kwa wafanyabiashara ambao nao huwauzia wananchi kwa bei kubwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa Dawasa, alisema wakazi wengi wa Magomeni, Vingunguti walishangaa kuona mabomba yao yakitoa maji baada ya kukosa huduma hiyo kwa takriban miaka mitatu.

Huduma hiyo ilirudishwa katika eneo hilo baada ya Dawasa kugundua wizi huo na kuunganisha upya.

Comments

Popular Posts