7 wauawa Saudi Arabia kwa wizi wa mabavu
ukataji vichwa Saudi Arabia
Watu 7 waliotuhumiwa kwa kosa la
wizi wa kimabavu wameuawa nchini Saudi Arabia licha ya tetesi kutoka
kwa wanaharakati wa haki za binadamu.
Duru zimearifu kuwa washukiwa hao waliuawa
katika mji wa Abha, kusini mwa nchi. Walimiminiwa risasi badala ya
kukatwa vichwa kama ilivyokuwa ada nchini humo.Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelalamika kuwa watu hao walitolewa hukumu kwa makosa waliofanya wakiwa chini ya miaka kumi na nane.
Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa zaidi ya watu 70 wameuawa na serikali nchini Saudi Arabia mwaka wa 2012 pekee

Comments
Post a Comment