Aliyemtukana Spika kwa simu kizimbani
Spika wa Bunge Anne Makinda
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alitoa taarifa hiyo jana kwenye vyombo vya habari.
Alisema mtu huyo alikamatwa Februari 12, mwaka huu, eneo la Shule ya Sekondari ya City iliyopo Area A, mjini hapa.
Bila kutaja matusi yaliyotumwa na mtuhumiwa huyo, Misime alisema,
mtuhumiwa huyo alitumia simu yake ya mkononi yenye namba 0763-448556
kutuma ujumbe huo wa matusi.
Alisema mtuhumiwa huyo ambaye amekana mashtaka hayo alifikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini, juzi na kesi yake
imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu itakapotajwa tena.
Kamanda Misime aliwataka wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuacha kutumia
simu zao za mkononi kwa kutuma ujumbe wa matusi na vitisho kwa watu
wengine.
Alisisitiza kuwa atakayekamatwa kwa tuhuma hizo atafikishwa katika vyombo vya sheria.
Kutukanwa kwa viongozi hao wa Bunge, kulifuatia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza namba za Spika na Naibu
wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Dar es Salaam ili
wawashinikize wajiuzulu.
Siku moja baada ya mkutano huo, chanzo kilicho karibu na Spika
Anne Makinda , kilisema jumla ya simu 200 zilipigwa kwa ajili ya
kumtukana.

Comments
Post a Comment