ANGALIA PICHA 6 ZA KWA BABU WA LOLIONDO IKIWEMO NYUMBA ANAYOJENGA NA KIBANDA CHA KUTOLEA DAWA
Hiki
ndio kibanda ambacho kinatumika kuhifadhi kikombe cha babu na kukigawa
kwa wanaotaka kunywa, zamani watu wakiwa wengi vikombe mpaka elfu 17-18
vilikua vinatoka kwa siku ila kwa sasa hawazidi watu 20, nimeongea na
kijana anaemsaidia babu kazi jana jioni.
Hii
ndio nyumba nyingine anayoijenga Babu wa Loliondo pembeni ya nyumba
anayoishi, alikanusha kuhusu kujenga majumba ya kifahari akasema hii
ndio nyumba pekee anayoijenga na ndio nyumba ya pili kuijenga toka
ameanza kutoa kikombe, ni ya vyumba vitatu na ni maalum kwa ajili ya
Wafanyakazi wake wanaomsaidia kwa ajili ya tukio kubwa alilolitangaza
linakuja karibuni.

Comments
Post a Comment