 |
| Mwenyekiti wa bongo movie Vicent kigosi (Ray) katika pozi |
Wale mastaa wa filamu nnchini tanzania Vicent kigosi Ray,Jacob
Stephan Jb,Irene uwoya,na yule king wa vichekesho nchini King Majuto kwa
pamoja wanatarajiwa kutua nchini rwanda kwa mualiko rasmi uliowataka
kwenda nchini humo.
Wasanii hao wamepata mualiko huo
kutokana na nchi hiyo kuzikubali sana kazi za wasanii watanzania na
kuona njia pekee ni kuwaita kwaajili ya kuwapa nguvu wasanii
wao,Akizungumza na Jamii leo huko kigali kwa njia ya simu Ndwimana
Ngikonwa ambaye ni mmoja wa mapromota wa nchi hiyo amesema yeye
anawafahamu sana wasanii hao na amefurahishwa sana na ujio wao kwani
itasaidia kuleta changamoto kwa wasanii wao.
 |
| King Majuto atakuwepo |
 |
| Jacob stephan Jb atakuwepo pia |
Promota huyo
ambaye inasemekana alishawahi kuwachukua wanamuziki kibao toka bongo
kwenda kupiga shoo huko kigali anaendelea kusema kuwa kama wasanii hao
watakubaliana nae atawapa dili jingine mara baada yakumaliza kazi
iliyowapeleka, Tulipomuuliza kama anahusika na safari hiyo alikana
nakusema hapana ila anajua mchongo wote na kuendelea kusema kuwa
hakujiingiza kwenye inshu hiyo kwani imekaa ki serekali zaidi bila
kufafanua maana yake.
 |
| Uwoya na Jb katka pozi wakati wakirekodi filamu |
Jamii leotz ilipomalizana na
promota huyo ilimuendea hewani Jb kama mmoja wasanii waliotajwa katika
safari hiyo kutaka kujua ukweli wa habari hizi na alipopatikana alisema
,Ni
kweli kaka tunasafari ya huko ila mengi mpigie Ray kwasababu yeye ni
mwenyekiti wa bongo movie atakueleza mengi zaidi kama kiongozi wetu
Mwandishi wa blogu hii alitaka kujua kama safari yenyewe ni kweli inahusu mwaliko
wa serekali ambapo Jb alijibu kwa kifupi yote mtajulishwa na ray,
 |
| Ray na Uwoya katika picha za filamu ya PRETTY GIRL |
Alipomalizana na jb moja kwa moja Mwandishi wa blogu alimuendea hewani
msanii Vicent kigosi ambae ni mwenyekiti wa bongo movie kwa sasa na
kumuuliza kama yeye na vijana wake wana safari ya kigali nchini Rwanda.
Nae kama jb alikiri kuwa na safari hiyo na hapo ndipo Jamii leotz
ilipotaka kujua kinachowapeleka rwanda ambapo ray alisema
Ni
safari ya kawaida kaka unajua kwa sasa tunamshukuru mungu sana kwani
imefika hatua nchi jiran wanaamini sisi tunaweza kuwa chachu ya wasanii
wao kufanya vizuri katika filamu na hili limefanya tuitwe huko.
Tulipotaka kujua kama safari hii inahusisha serekali ray alicheka na kusema
Unajua
wenzetu ni tofauti na sisi wao kila kitu kinaenda kisheria huwezi
kufanya jambo mpaka chama kijue na kikishajua ni serekali japo sisi kama
sisi tutakutana viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa sababu nnchi
nzima ya rwanda imeshajua na imejiandaa kwa ajili yetu na imeandaa
mapokezi makubwa sana wanasema wanataka yavunje yazidi yale ya congo
niliyoyafanya nikiwa na swahiba marehemu steven kanumba.
 |
| Uwoya katika pozi |
Ray
alipoulizwa wataondoka lini kuelekea huko amesema kesho nitakupa jibu
kaka maana mambo yote yapo poa ila elewa muda wowote kuanzia leo
tutaondoka Nae kiongozi wa msafara amesema kuwa katika ziara hiyo
wasanii hao wanatarajia kukutana na mheshimiwa raisi na kumuelezea
kiundani wigo wa sanaa na nini kifanyike kuinua sanaa ya rwanda Ray
amewataja wasani atakao ongozana nao kuwa ni pamoja na Irene uwoya
,,Jacob Stephen Jb, na Mzee King Majuto Jamii leotz inawatakia kila
la kheri na kuwaomba waitangaze tanzania kila dakika watakayopata
nafasi hiyo
Comments
Post a Comment