ANGALIA PICHA ZA RAIS KIKWETE..........DENMARK
Msafara wa Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt ukikaribia lango la Mashariki la Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimueleza Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt aina ya mti ataoupanda leo Ikulu
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Sanga na
maofisa wengine waandamizi wakati akimsibiri mgeni wake
hadi
a12: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa
Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt wakiingia Ikulu huku wakishangiliwa
Shughuli ya kwanza ya Waziri Mkuu huyo wa Denmark leo asubuhi itakuwa kukutana kwa mazungumzo ya faragha na rasmi na Rais Kikwete Ikulu, Dar Es Salaam, mazungumzo ambayo yatafuatiwa na viongozi hao wawili kuzungumza na waandishi wa habari. Baadaye mchana, Bi. Helle Thorning-Schmidt atatoa mhadhara kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na jioni atahudhuria na dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa na Rais Kikwete.
Keshokutwa, Bi. Thorning-Schmidt atakwenda Arusha ambako atatembelea Mahakama Maalum ya Uhalifu ya Rwanda (ICTR), atatembelea Kijiji cha Wamasai cha Lepurko na baadaye kutembelea shamba la kahawa linalomilikiwa na Bwana Christian Jespen.
Ijumaa, mama huyu atatembelea Hospitali ya Wilaya ya Mbulu na kituo cha kufundishia wauguzi cha hospitali hiyo, atatembelea Mbuga ya Wanyama ya Tarangire, atatembelea Makao Makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na kukutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Mheshimiwa Richard Sezibera kabla ya kutembelea Kituo cha Mafunzo cha Action Aid kinachoendeshwa na Serikali ya Denmark cha MS-TCDC. Mheshimiwa Helle Thornig-Schimidt ataondoka usiku wa siku hiyo kurejea nyumban

Comments
Post a Comment