ANGALIA PICHA ZA RAY,JB,KING MAJUTO,WALIVYOPATA MAPOKEZI YA NGUVU RWANDA
| Msanii vicent kigosi (Ray) |
wasanii ray,jb,uwoya na king majuto ambao walikuwa safarini huko nchini
rwanda wameongea na mwandishi wa blogu hii wakiwa huko nchini rwanda na kueleza
kufurahishwa kwao na ziara yao na kuwashukuru wanyarwanda kwa mapokezi
makubwa ambayo binafsi hawakuyategemea.
Akizungumza na sisi kwa njia ya simu kiongozi wa bongo movie Vicent
kigosi Ray Amesema kuwa binafsi amefurahishwa na mapokezi ya wanyarwanda
na kuongeza kuwa ni watu wa karimu sana na ameahidi kushirikiana nao
kila watakapo muhitaji kwani amegundua vipaji vingi nchini humo.
| Msanii Irene Uwoya |
![]() |
| Msanii King majuto |
Kwa upande wa msanii Jacobu stephasn au Jb Amesema katika maisha yake
aliamini watu wa rwanda ni wakorofi na bado vita inaendelea lakini
ameshangazwa na mapokezi waliyoyapata na utulivu uliopo nchini rwanda.



Comments
Post a Comment