BAADA YA "KIGOMA ALL STARS" SASA NI ZAMU YA "MARA ALL STARS" KUFANYIWA MCHAKATO.
| Mkurugenzi wa kampuni ya MAG Promotion entertainment East Africa ili Maganya Fadhili akiongea na Mwandishi wa blogu hii kuhusiana na wazo lake la kuanzisha mara all starz |
.
KAMPUNI ya Mag Promotions na Entertainment East Africa
inakusudia kuwaunganisha wasanii wote wa muziki wa Injili na wale wa kizazi
kipya wanaotokea mkoani Mara ikiwa ni juhudi za kuiga mfano wa wasanii wanaunda
kundi la Kigoma All Stars.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa kampuni
hiyo, Maganya Fadhili alisema kuwa kuwa kampuni yake inajishughulisha na masuala
ya kuwapromoti wasanii mbalimbali nchini ameona ni bora awaunganishe wasanii
wanaotoka mkoani Mara kwa kuzingatia na yeye ni mzaliwa wa mkoani humo.
Fadhili,ambaye alivunja rekodi ya kumleta msanii Jose
Chamilione mwaka 2002 na kumtembeza mikoa 17 hapa nchini alisema kwamba huu ni
wakati wa wasanii kutoka mkoani Mara kama Judith Wambura”Lady Jay Dee” kuungana
kwa pamoja ili kujiletea maendeleo.
Hatahivyo,alisema tayari alishafanya utaratibu wa
kuwasiliana na baadhi ya wasanii
wanaotoka mkoani ambapo wamemsapoti na kusisitiza kuwa pindi utaratibu
ukishakamilika watakubalina kufanya kazi kwa ushirikiano.
Alitoa wito kwa mapromota wa kazi za wasanii wanaotoka
mkoani Mara kama Jospeh Kusaga na Chief Kiumbe kumsapoti katika harakati hizo
ili kuutangaza mkoa wa Mara aliodai una fursa nyingi za kiuchumi.
“Natoa wito kwa mapromota mbalimbali wa kazi za muziki kama
Kusaga na Chief Kiumbe wanaotoka mkoani Mara tuunganishe nguvu kwa pamoja ili
kuutangaza mkoa wa Mara”alisema Fadhil

Comments
Post a Comment