Denmark kusaidia Monduli milioni 50
Mbunge wa wilaya ya Monduli, Edward Lowassa.
Ahadi hiyo imetolewa jana na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning
Schmidt, wakati alipotembelea boma la kimasai lililopo kijiji cha
Nanja.
Alisema anaamini bwawa hilo litanufaisha vijiji vya kata ya Lepurko yenye vijiji vya Nanja na Mti mmoja.
Helle alisema serikali yake imesikitishwa sana kuona kinamama wa
jamii ya wafugaji wanatembea umbali mrefu kusaka maji ambayo si salama.
“Kinamama bado wanapata shida wanapokuwa njiani kutafuta maji ya
kunywa, bado wanakumbana na wanyama wakali kama Simba na wengine
kujeruhiwa na baadhi kufariki,” alisema.
Alisema anaamini kukamilika kwa bwawa hilo kutawaondolea adha ya maji waliyonayo na kutembea mwendo mrefu kutafuta maji.
Helle alisema serikali yake inajali maendeleo ya wanawake na kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo.
Alisema hapendezwi kuona akina mama, wakiwa na watoto mgongoni,
wanakwenda kutafuta maji kwa mwendo mrefu, hivyo atashughulikia tatizo
hilo haraka.
Akiongea kwa niaba ya wenzake, Esuphat Laizer, alisema kuwa kilio
cha ukosefu wa maji cha miaka mingi na kutokana na adha hiyo, wamepoteza
mwezao mmoja kwa kuliwa na simba kwa sababu ya kutafuta maji na wengine
kujeruhiwa.

Comments
Post a Comment