DK.SHEIN HOI KWA .............ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein
Hayo yalisemwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, katika ziara yake baada ya kupokea taarifa ya utekeklezaji majukumu ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dk. Shein alisema idadi ya watu katika mkoa huo inaongezeka kwa kasi ya watu 506,907 kutoka 391,002 mwaka 2002.
Alisema kwa mujibu wa wataalam wa takwimu, kumekuwapo na ongezeko la watu ambalo halilingani na mahitaji ya huduma muhimu za jamii na kuathiri wakazi wake.
“Huduma nyingi kama vile maji na umeme hazitoshelezi...lakini serikali inachukua jitihada za kuimarisha huduma hizo,” alisema Dk. Shein.
Rais wa Zanzibar ambaye yuko katika ziara ya siku mbili katika mkoa mjini Magharibi, alikagua mradi wa uchimbaji visima eneo la Chumbuni na mradi wa umeme Welezo.
Akiwa katika mradi wa maji wa uchimbaji visima Chumbuni Wilaya Mjini, Dk. Shein aliutaka uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa) kuhakikisha kuwa unakuwapo usalama wa vyanzo na miradi ya maji ikiwamo kufanya jitihada za kuwaelimisha wananchi kuvilinda pamoja na vifaa vya miradi.
Upande wake, Mkurungezi Mkuu wa Zawa, Dk. Mustafa Ali Garu alimueleza Rais na ujumbe wake kuwa mradi wa visima tisa utasadia kuongeza uzalishaji maji katika vyanzo vya maji Mwanyanya na Mtoni Zanzibar.
Kuhusu utekelezaji wa mradi huo, alisema visima vitano tayari vimechimbwa Chumbuni na Saateni tangu kuanza kwa mradi huo Agosti, 2011.
Wakati huo huo, Dk. Shein ametembelea mradi wa uimarishaji huduma za umeme eneo la Welezo, Wilaya ya Mjini na kuona hatua zilizofikiwa.
Dk. Shein alipongeza hatua hizo zilizofikiwa hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma ya uhakika ya umeme kwa wananchi hasa baada ya kukamilika kwa mradi wa njia mpya ya kusafirisha umeme Zanzibar kutoka Tanzania bara.
Kituo hicho cha umeme ni miongoni mwa vituo vitatu vya kupokea umeme na mradi umegharimu Shilingi bilioni saba.
Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), Hassan Salum, alisema kituo cha Welezo, kitasaidia kutoa huduma ya umeme kwa maeneo ya Kilimahewa na maeneo ya kusini yakiwemo Mwera, Bambi na Koani Mkoa wa Kusini Unguja

Comments
Post a Comment