GATTUSO KUSTAAFU SOKA JUNE
.
KIUNGO nyota wa zamani
wa kimataifa wa Italia na klabu ya AC Milan, Gennaro Gattuso amesema
anatarajia kustaafu rasmi kucheza soka katika kipindi cha majira ya
kiangazi ili aweze kuhamishia nguvu zake kwenye ukocha. Gattuso
mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya FC Sion
ya Switzerland amedai anadhani wakati wa kutundika daruga umefika baada
ya kucheza kwa kipindi cha miaka 18. Nguli
huyo amesema mara baada ya kuacha kucheza soka anataka kujitolea kwa
nguvu zake zote katika kazi yake mpya ya ukocha ili aweze kupata
mafanikio kama ilivyokuwa wakati akicheza soka. Nyota
huyo aliendelea kudai kuwa amepata uzoefu wa kutosha wakati akiwa
mchezaji chini ya makocha Marcello Lippi na Carlo Ancelotti kwani
walikuwa walimu wazuri kwake wakati akiwa Milan. FC
Sion ambayo kwasasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu
nchini Switzerland maarufu kama Swiss Super League wanatarajia kusafiri
kwenda Geneve Jumapili kupambana na timu ya Young Boys.


Comments
Post a Comment