Gavana aliyeiba pesa asamehewa Nigeria
ramani ya Nigeria
Vyombo vya sheria nchini Nigeria
vimemsamehea gavana wa zamani Diepreye Alamieyeseigha aliyeshutumiwa
kuiba mamilioni ya dola kutoka kwa serikali. Msamaha huo ulitolewa na
baraza la serikali, linalojumuisha rais Goodluck Jonathan ambaye aliwahi
kuhudumu chini ya bwana Diepreye
.Mmoja wa waandishi wa blogu hii nchini humo amesema kuwa hatua hiyo, ambayo imepingwa vikali na wanaharakati dhidi ya ufisadi, inamaana kuwa bwana Diepreye ataruhusiwa kuwania wadhifa wa kisiasa.
Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Bayelsa ambaye alitiwa nguvuni nchini Uingereza mwaka wa 2005 alikwepa kifungo kwa kukimbilia nchini Nigeria akiwa amevaa mavazi ya kike.
Amehudumu siku mbili tu ya kifungo cha miaka miwili aliyohukumiwa

Comments
Post a Comment