Skip to main content
GUARDIOLA ATAKUWA CHINI YA SHINIKIZO KUBWA BAYERN - BECKENBAUER.
NGULI wa soka wa zamani
nchini Ujerumani, Franz Beckenbauer amedai kuwa meneja mtarajiwa wa
klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola atakuwa chini ya shinikizo kubwa
kufikia mafanikio yaliyowekwa msimu huu na meneja wa sasa Jupp
Heynckes. Kocha
huyo wa zamani wa Barcelona anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa Bayern
Julai mosi mwaka huu lakini Heynckes ambaye ataondoka mwishoni mwa
msimu ametengeneza pengo kubwa katika mbio za ubingwa wa Bundesliga kitu
ambacho kinamuogopesha Beckernbauer. Bayern
kwasasa inaongoza Bundesliga kwa tofauti ya alama 20 baada ya kupambana
kutoka nyuma mara mbili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya
Fortuna Duesseldorf Jumamosi iliyopita. Klabu
hiyo kama ikishinda mechi tatu za ligi zinazofuata itakuwa tayari
wametawazwa mabingwa wapya wa Bundesliga hiyo ikiwa ni mara ya 23
kushinda taji hilo. Nguli
huyo anadai kuwa kila mtu anafikiri mambo yanaweza kubadilika kwa klabu
hiyo wakati Guardiola atapoanza kufundisha hivyo kama timu itachukua
ubingwa kwa tofauti ndogo ya alama kuliko msimu huu watu wanaweza kukosa
imani naye. Maneno
ya nguli huyo yaliungwa mkono pia na rais wa Bayern Uli Hoeness ambaye
amesema anafikiri timu hiyo itakuwa bingwa wa ligi msimu huu hivyo
shinikizo kwa Guardiola na klabu litakuwa kubwa.
Comments
Post a Comment