Imamu auawa Zanzibar




IMAMU Khamis Ali [60] wa msikiti wa Mwakaje, ameuawa kwa kupigwa na mapanga na watu ambao hawajafahamika akiwa shambani kwake


Imamu huyo aliuawa na watu hao ambao walivamia shambani kwake kwa lengo la kuiba mazao katika shamba hilo

Imedaiwa imamu huyo alikwenda shambani kwake huko maeneo ya Kitope Kaskazini Unguja lililopo shamba hilo

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bw. Ahmada Abdallah amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya mchana akiwa shambani humo

Amebainisha kamanda kuwa, wakati alipoingia shambani humo alikuta watu hao wakiiba nazi ndipo watu hao wakamvamia na kumpa dozi ya kumpa kichapo kwa mapanga na kupeleka kifo chake

Tayari mazishi ya kiongozi huyo yamefanyika jana na uchunguzi wa wauaji unaendelea
Mji wa Zanzibar umegubwika na machafuko ya mauaji ya viongozi wa kidini na kujeruhiwa na watu ambao hawafahamiki jambo ambalo linaleta sintofahamu visiwani humo

Hadi sasa matukio ya mauaji ya viongozi wa kidini visiwani humo yanafikia matatu na moja kujeruhiwa

Tukio la kwanza la mauaji ni pale Padri Ambrose Mkenda ambaye aliuawa kwa kupigwa mapanga akiwa nyumbani kwake, tukio la pili ni kuuawa kwa Padri Mushi tukio lilitokea wiki iliyopita ambalo hadi sasa vuguvugu hazijaisha na wauaji hawajapatikana

Tukio la tatu la mauaji ni hili lililobeba habari hii na tukio lingine ni kujeruhiwa kwa Shekhe Suleiman Soraga aliyemwagiwa tindikali akiwa mazoezini majira ya asubuhi na watu wasiojulikana na hali yake ilikuwa mbaya na aliweza kusafirishwa kwenda nchini India kwa matibabu na sasa amerudi nchini na anaendelea vizur

Comments

Popular Posts