KESI MAANDAMANO YA WAISLAMU:Shahidi: Nilikamatwa nikitoka msikitini
Wakili wa Utetezi, Mohammed Tibanyendera
.
Shahidi huyo wa 31 wa upande wa utetezi, Bakari Athumani, alidai
kwamba siku ya tukio, alikuwa anatoka msikitini kuelekea Kidongo
Chekundu, lakini alipofika mtaa wa Uhuru na Mnazi Mmoja, alikamatwa na
polisi bila kujua kosa lake.
“Nilikuwapo kwenye kongamano la Kiislamu lililofanyika mwishoni
mwa Februari Temeke ambapo Shekh Juma Bungo, aliwasisitiza Waislamu wote
kuandamana Februari 15, mwaka huu endapo Sheikh Ponda Issa Ponda,
hatapewa dhamana. Lakini mimi binafsi sikuandamana kwa sababu sipendi
kufanya hivyo,’’ alisema Athumani.
Alitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Sundi Fimbo.
Washitakiwa wengine wa upande huo wa utetezi walidai kwa nyakati
tofauti kuwa hawamfahamu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) cheo chake wala
hawajui ofisi yake ilipo.
Wakili wa Utetezi, Mohammed Tibanyendera, aliyewaongoza washtakiwa.
Washtakiwa hao kwa nyakati tofauti walidai kuwa hawamfahamu Sheikh
Ponda wala hawafahamu kesi yoyote kuhusiana na Masheikh inayoendelea
mahakamani hapo.
Ushahidi wa upaande wa utetezi katika kesi hiyo utaendelea kusikilizwa leo.

Comments
Post a Comment