LULU ASEMA KWASASA HATOONEKANA KATIKA FILAMU...AWA MTU WA BIBILIA NA VITABU
Msanii wa filamu nchini elizabeth michael amesema kuwa kwa sasa
hafikirii kufanya filamu badala yake ameamua kujikita katika maswala
yake ya elimu na kwasasa amejipanga kwa mambo ya elimu tu.
Wakizungumza na jamiileotz mapema hii leo wadau wa filamu
wameonyesha kumtaka lulu arudi na kuonyesha makali yake katika filamu ambapo wadau hao wameonyesha kumkumbuka sana msanii huyo mwenye makeke awapo mbele ya camera.
Msanii huyu kwasasa yupo mafichoni akijipanga na wadau na wapenzi wake
wameonyesha dhahiri kumiss sana lulu hadi wengine kusema wanataka
kumuona tu hata kwa kawaida kama kwenye filamu
imeshindikana,jamiileotz imeongea na baadhi ya wadau wa filamu
maeneo ya karikoo katika maduka ya kanda na kubaini kuwa watu wamem
misss sana lulu kwani kwa dakika chache katika duka moja la kanda maeneo
ya karikoo, jamiileotz imeshuhudia watu kibao wakija katika duka
hilo na kuuliza kama lulu ameshatowa filamu mpya.
Baada ya kukutana na wadau hao jamiileotz ilibisha hodi katika nyumba anayoishi lulu kwa msaada wa msanii Mahsen Hawadhi Dk Cheni aliyetusaidia kumpata lulu tulipoonana na lulu tulimuuliza juu ya kukaa kwake kimya ambapo alisema Najua kama wadau wamenimiss ila ninawaomba wanivumilie kwasasa kwani bado sijakaa vizuri najipanga kwaajili ya mambo yangu ya kurudi shule kwani nimejifunza mengi sana na nimejipanga sana katika mambo yangu ya kielimu,Alisemasa lulu.
Kwasasa msaanii huyo ameonekana kuwa mtulivu sana kwani muda mwingi anaonekana kushika biblia na kusoma novo kitu ambacho kinafanya kila anayemjua lulu kushangazwa na staili hii ya maisha mapya ya lulu na kumshangaa lulu huyu si yule wa zamani,na kufanya watu wakiri kuwa mwanadada lulu kabadilika sana,Jamiileotz inampongeza lulu kwakukumbuka na kuamua kurudi shule na kwakutulia na kujipanga tena kwani tunaamini bado anayo nafasi kubwa sana ya kubadili maisha yake

Comments
Post a Comment