MASHABIKI 21 WAHUKUMIWA KIFO MISRI BAADA YA VURUGU ZA PORT SAID.
MAHAKAMA nchini Misri
imewahukumu kifo mashabiki wa soka 21 waliokuwa vinara wa vurugu
zilizotokea uwanjani huko jijini Port Said mwaka uliopita kesi ambayo
ilizua mapigano makali katika mji huo uliopo katika mto wa Suez. Mauaji
hayo yalitokea Februari mwaka jana mwishoni mwa mechi kati ya Al-Ahly
ya jijini Cairo na wenyeji wa mji huo timu ya Al-Masry. Watazamaji
walikanyakagana wakati wakijaribu kutoka uwanjani baada ya mashabiki wa
Al-Masry kuvamia uwanjani na kuanza kupigana na wengine kurushwa nje ya
uzio. Akitaja
majina ya watuhumiwa 21 jaji amesema mahakama hiyo imeridhishwa na
ushahidi uliotolewa na hivyo kuwahukumu mashabiki hao kunyongwa hadi
kufa. Mbali na
hao mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine watano kifungo cha maisha
jela kwa vurugu hizo huku wengine 28 kati ya mashabiki 73 waliofikishwa
mahakamani hapo wamepewa vifungo vya muda mfup


Comments
Post a Comment