Mbunge Aliyeanguka Kikaoni Afariki Dunia Muhimbili

Mbunge Salim Hemed Khamis akiwa amebebwa baada ya kuanguka kikaoni.
MBUNGE wa Jimbo la Chambani, Pemba Kisiwani Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Salim Hemed Khamis, alianguka ghafla jana wakati akihudhuria vikao vya kamati za Bunge katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba mbunge huyo amefariki dunia alipokuwa akiendelea kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo alipelekwa tangu jana afya yake ilipobadilika ghafla kikaoni.
Taarifa zaidi zimesema hadi sasa taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanywa kwa kushirikiana na pande zote husika. Mtandao huu utakuletea taarifa kamili hapo baadaye. Mungu ailaze roho ya marehemu Salim Hemed Khamis mahali pema peponi. Amen

Comments