Moto wasababisha hasara bilioni 25/- mgodi wa Geita

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Leonard Paul
Moto mkubwa umeibuka ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 25.
Hata hivyo, chanzo cha moto huo hakijafahamika na uchunguzi tayari umeanza. Aidha, tukio hilo lililotokea Februari 26, mwaka huu, saa 10:00 jioni, limegubikwa na usiri mkubwa kutokana na vyombo vya habari kutoruhusiwa kuingia ndani ya mgodi huo.
Majengo mawili likiwamo ghala kuu la kuhifadhia vipuri na vifaa vya aina mbalimbali viliteketezwa kwa moto huo.
Mkurugenzi wa mgodi huo, Garry Davies, alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula, mwishoni mwa wiki kuwa inakadiriwa thamani ya mali iliyoteketezwa na moto huo ni dola milioni 15 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 25).
Magagula alitembelea mgodi huo akiwa amefuatana na wajumbe  wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita.
Baadhi ya mashududa walioshuhudia tukio hilo walidai kuwa moto huo ulikuwa mkali na kusababisha watu washindwe kuuzima.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Leonard Paul, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo

Comments

Popular Posts