Polisi Temeke walalamikiwa kuwa chanzo cha uhalifu
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile
Malalamiko hayo yalitolewa na wananchi wa kata hiyo mwishoni mwa wiki katika mkutano uliowakutanisha Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, Diwani wa kata hiyo, John Gama, viongozi wa kata na mitaa na Jeshi la Polisi.
Mmoja wa wananchi, Mariam Chano, alidai kuwa Jeshi la Polisi linachangia uvunjifu wa amani kutokana na kutofika maeneo ya matukio ya uhalifu kwa wakati.
Alisema wananchi wamekuwa wakivamiwa na wengine kuibiwa, lakini Jeshi la Polisi halifiki eneo la tukio wala kufanya doria, kitendo ambacho alisema kinawapa nguvu wahalifu.
Aliongeza kuwa vikundi vya ulinzi shirikishi katika kata hiyo havipati ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi pindi unapohitaji msaad.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Chamazi, Gassan Mtinya, alisema shutuma hizo si za ukweli na kumtaka mtu yeyote mwenye malalamiko afike kituo cha polisi kwa ajili ya ufafanuzi zaidi

Comments
Post a Comment