POLISI WASHITUMIWA ...........SHEIK PONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda
Mashahidi saba wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda (54) na wenzake 49, wamedai mahakamani kwamba askari polisi waliwavamia wakiwa kwenye ibada na kuvunja milango na madirisha ya msikiti wa Chang’ombe Marcas, jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, walidai kuwa baada ya kuvunja milango na madirisha ya msikiti huo, waliingia na viatu na kuwapiga kwa virungu na kuwasababishia baadhi yao majeraha.
Kuluthumu Mfaume (45), shahidi wa kwanza wa utetezi alitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Alidai kuwa kundi la askari waliowavamia msikitini hapo lilikuwa na wanaume bila kuwapo mwanamke hata mmoja.

“Askari wote waliotuvamia walikuwa na sare za Jeshi la Polisi, wanaume tupu hakuwepo mwanamke hata mmoja… walifanya uchafu mkubwa sana, waliingia bila kuvua viatu,” alidai.

Aidha alidai kuwa haifahamu na halitambui Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).
Shahidi wa pili, Zainabu Mohamed (50 na wa tatu, Zaidan Yusufu, walidai kuwa polisi walivunja milango na madirisha ya msikiti huo na kuwatoa nje huku wakiwasindikiza kwa marungu.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa utetezi leo.
Mbali na Ponda washtakiwa wengine ni, Sheikh Mukadam Saleh, Kuluthumu Mohamed, Zaldah Yusuph, Juma Mpanga, Farida Lukoko, Adamu Makilika, Athum Salim, Seleman Wajumbe, Salum Juma, Salum Mkwasu na Ramha Hamza.

Wengine ni, Halima Abas, Maua Mdumila, Fatihiya Habibu, Hussein Ally, Shaban Ramadhani, Hamis Mohamed, Rashid Ramadhani, Yusuph Penza, Alawi Alawi, Ramadhani Mlali, Omary Ismaili, Salma Abduratifu, Khalidi Abdallah, Said Rashid, Feswali Bakari, Issa Wahabu, Ally Mohamed, Mohamed Ramadhani, Abdallah Senza, Juma Hassani na Mwanaomary Makuka.

Pia wamo Omary Bakari, Hamza Ramadhani, Ayubu Juma,Maulid Namdeka, Farahan Jamal, Smalehes Mdulidi, Jumanne Mussa, Salum Mohamed, Hamis Halidi, Dite Bilali, Amiri Said, Juma Yassin, Athuman Rashid, Rukia Yusuph, Abubakari Juma na Ally Salehe.

Comments

Popular Posts