RAIS KIKWETE AKIWA NA FURAHA NA MWANAYE RIDHIWANI KATIKA MOJA YA SHEREHE ZA KIISLAMU


Dr Jakaya MK Kikwete,
Unatawala katika kipindi kigumu sana!!
1.kipindi ambacho UDINI umetamalaki kiasi kwamba unatamani hata kuuficha uislamu wako kwa shutma nyingi dhidi yako mpaka inapotokea mtafaruku baina ya waislamu na wakristo inabidi uende kuzuru makanisa huku ukiipita misikiti, na hata kama ni misiba inabidi ukamzike padre na Askofu huku masheikh wakizikana wenyewe- bado uko Imara
2.Kipindi ambacho unalalamikiwa kwa kuyakalia kimya majanga kama vile muandishi wa habari kumwagiwa Tindikali, muandishi kupigwa bobu, kutekwa kwa maDr(mabwepande), kutekwa kwa masheikh(znz), kumwagiwa tindikali kwa masheikh(znz), wasanii kukuimba(eti Mr President), mkuu wa mkoa kupiga mtu Risasi(Ditto), wanajisahau kua kuna vitengo vya kushughulikia hayo, hawajui uraisi ni taasisi- bado uko imara
3.Vyama vya Siasa vinakuzonga mara ooh ni dhaifu, mara huna maamuzi magumu nk nk cha ajabu ukiwapa nafasi ya umatemate wanatulia(mbatia, CUF, nk) hata hawa wanaleta fujo ukiwapoza tu watakulamba miguu maana naona unapowaalikaga Ikulu Furaha wanayokuaga nayo!- bado uko imara
4.Migomo ya wanafunzi, waalimu, wazee wa jumuiya ya afrika mashariki, madaktari, madereva, nk nk Eti wanata wewe ulipe kwa pesa zako za madafu, haiwezekani bhana_bado uko imara
5.Dini flani miaka flani zilikuita chaguo la Mungu ghafla ulipofanya kazi zako ipaswavyo wakakuita mdini na haufai tena, suala la kodi kwa taasisi za dini lilipogusa maslah ya ulaji wa baadhi ya viongozi ukasakamwa tena- bado uko imara
6.Mwanao Ridhiwani kua tajiri ni haramu eti unamlimbikizia ila wao watoto wao na baba zao walivyotufanya ni sawa tu, lakini bado uko Imara
7.Hii sasa ndo balaa, mpaka baadhi ya wanachama wenzio walitaka kukupiga chini uenyekiti wa chama lakini ukapambana nao na sumu yako wakaionja kwenye hotuba yako na kwny CC mpya- uko imara
8.Wanafunzi kufeli na maalbino kuuwawa walitaka kukuandama tena
UKO IMARA SANA, ulipochokozwa na kale ka nchi ka jirani ukataka kukaadabisha kakaingia mitini wakakuona jembe, ulipokua mwenyekiti wa ule umoja wa nanihii Afrika wakakuona jembe, na ukiendelea na msimamo wako huo watazidi kukubali kua wewe ni jembe lenye mpini wake, hiki kipindi sio kile cha Tuzienzi fikra za Kambarage( hapakua na Uhuru wa Vyombo vya habari, hata hawa japo wnw degree feki za tena kuungaunga hawakua wengi, ukileta mgomo hata maiti yako sijui kama itapatikana)
I'M PROUD OF YOU Luteni!!
Mwingizi.

Comments

Popular Posts