ROSE NDAUKA AFUNGUKA NA KUKIRI KUWA NA MUME WA MTU ..AOMBA MSAMAHA NA KUAHIDI HAITORUDIA TENA

Rose Ndauka katika Pozi

 
Msanii mahiri wa filamu nchini Tanzania Rose ndauka amejikuta akiwekwa mtu kati na kukubali tuhuma za kutembea na mume wa mtu huku akionyesha kujutia alichokifanya na kudai hatorudia tena na kuahidi kuwa haitatokea tena.
Rose amejikuta katika wakati mgumu pale alipokuwa akihojiwa na Zamaradi mketema katika kipindi cha movie leo na kujikuta akikubali kuwa alishawahi kuwa na mume wa mtu.
Kazi ilianza pale Rose alipopigiwa simu na zamaradi kutokana na filamu yake mpya inayotaka kutoka aliyomshirikisha Mohamed Mwikong,Hidaya Njaidi na Jamila Jalawi inayotarajiwa kutoka hivi karibuni
Baada ya kuulizwa kama filamu aliyoitengeneza ina mahusiano na maisha yake rose alisema kuwa haihusiani na hata kama itaonekana kuhusiana basi si sana.katika mahojiano hayo rose alionekana kushindwa kutetea hoja yake haswa pale alipobanwa na kujikuta anakubaliana na swali la zamaradi ,Ni kweli nilishawahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu lakini sikuwa na jua kama ni mume wa mtu na nilipojua kama ni mume wa mtu niliachana nae na ninaomba radhi kwa niliowaumiza kwa kipindi hicho na nina ahidi haitajitokeza tena na sirudii kwani huwa najisikia vibaya sana nikikumbuka kuwa nilifanya makosa kumuumiza mwanamke mwenzangu bila sababu.

Rose Ndauka katika Pozi


Wakati kipindi hicho kinaendea jamiileotz ilinua simu na kumpigia mwanadada huyo ila hakupokea simu na baada ya kurudia rudia ilipokelewa na msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Iren na kusema namba ni yake na hana ukaribu na ndaukana kwa hiyo tumekosea namba japo jamiileotz ilipomtafuta rafiki wa rose na kutaka namba ya rose alitutumia hiyo hiyo na hapo ndipo tulipoamua kumpigia mchumba wake ajulikanae kwa jina Malik ambae alipoambiwa anaongea na jamiileotz alisema nipo busy kaka nitakucheki na kukata simu

Comments