Sandra adaiwa kutelekeza mtoto

Msanii wa filamu Salama Salmin 'Sandra�
Msanii wa filamu Salama Salmin 'Sandra’ ameripotiwa Polisi katika kituo cha Kawe jijini Dar es salaam akidaiwa kumtelekeza mtoto wake wa miaka saba (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la pili katika shule ya Green Acres ya jijini Dar es salaam
.
Alipotafutwa kwa njia ya simu jana, msanii huyo alisema hawezi kumtelekeza mtoto wake bali uongozi wa shule ujibu ni kwanini umekaa na mtoto wake.
 
Licha ya kuripotiwa kumtelekeza mtoto huyo, Sandra na mzazi mwenzie aliyetajwa kwa jina moja la Dk. Rweikiza wanatakiwa kurudisha kwa uongozi wa shule hiyo sh. milioni 1.5 za malipo ya ada ya mwaka mmoja na miezi mitatu.
 
Akizungumza jana na waandishi wa habari shuleni hapo, Mkuu wa shule hiyo, Ashery Semu, alisema msanii huyo alimuacha mtoto huyo shuleni hapo akiwa hana mahitaji yoyote.  
 
“Huyu mtoto aliachwa hapa hana nguo, sare za shule zimechanika, hana sabuni, shuka, mswaki... ikabidi matron ampatie na tumekuwa tukiwaita wazazi wake kwa muda refu lakini hawaonyeshi kujali wala kufika hapa shuleni kuzungumzia suala la mtoto wao,” alisema.
 
Semu alisema baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na kupatiwa majibu ya kukatisha tamaa uongozi wa shule uliamua kufikisha suala hilo polisi.
 
Shauri limepewa namba KW/RB/2615/2013 ya kosa la kutelekeza mtoto
Alipomuuliza kuhusiana na madai ya fedha anazodaiwa, msanii huyo alikata simu na alipopigiwa tena simu iliita bila kupokelewa

Comments