Spika Makinda apangua kamati za Bunge
Spika wa Bunge, Anne Makinda
Katika ‘panguapangua’ hiyo, kamati hizo zimepunguzwa kutoka 18 za zamani na kubaki 17, pia wajumbe wake wamepangwa upya kwenye kamati mbalimbali.
Kamati zilizofutwa ni Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati ya Fedha na Uchumi.
Iliyomegwa ni iliyokuwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambayo baada ya kumegwa, zimeundwa kamati mbili mpya tofauti, ambazo kila moja inajitegemea.
Kamarti hizo, ni ya Ulinzi na Usalama, nay a Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Pia baada ya kuzifuta, Kamati ya Fedha na Uchumi, sehemu yake imemegwa na kuunganishwa kwenye Kamati ya Viwanda na Biashara, ambayo kwa sasa inajulikana kama “Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara”.
Kamati tatu mpya zilizoundwa ni pamoja na Kamati ya Bajeti, na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambazo hazikuwapo kabisa kwenye orodha ya kamati 18 za zamani.
Kamati nyingine zimeendelea kubaki kama zilivyokuwa katika orodha ya kamati za zamani.
Kwa mujibu wa tangazo linalohusu orodha ya uteuzi wa wajumbe wa kamati za Bunge, lililotolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge jana, hatua hiyo imechukuliwa na Spika kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na kanuni ya 113 ya kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007.
“Mamlaka aliyopewa Spika na kanuni ya 113 ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007, uteuzi wa wajumbe wa kamati kwa kipindi kilichobaki cha uhai wa Bunge hili sasa umekamilika kama ilivyo kwenye orodha,” ilieleza sehemu ya tangazo hilo.
Tangazo hilo lilieleza kuwa madhumuni ya kuwapanga upya wabunge kwenye kamati mbalimbali ni kuwapatia fursa kadri inavyowezekana kujipatia ujuzi na uzoefu wa shughuli za kamati tofauti na pia kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kanuni za 113 (5).
Tangazo hilo lilieleza kuwa uteuzi huo ulianza jana na leo utafanyika uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo.
Wajumbe wa kamati hizo walioteuliwa upya ni wafuatao:
KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE
Anne Makinda (Spika), Job Ndugai (Naibu Spika), Tundu Lissu, Andrew Chenge, Musa Azzan Zungu, Dk.Titus Kamani, Jenista Mhagama, William Ngeleja, Amina Abdallah Amour, James Mbatia, Hamad Rashid Mohammed, Jasson Rweikiza, Philipa Mturano, Anna Abdallah na Christopher Ole-Sendeka.
KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
Augustino Mrema, Riziki Omar Juma, Assumpter Mshama, Brigedia Jenerali (mstaafu)
Hassan Ngwilizi,Agripina Zaituni Buyogera, Said Nkumba, John Lwanji, Mchungaji Israel Natse, Kapteni John Chiligati, Betty Machangu, Said Arfi, Gosbert Blandes, Augostino Masele, Dk. Lucy Nkya na Rashid Ali Abdallah.
KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI
Said Suleiman Said, Ahmed Ali Salum, Maida Hamad Abdallah, Lediana Mung’ong’o ,Maria Hewa, Chiku Abwao, Omary Badwel, Mbarouk Salim Ali, Rashid Ali Omar, Lameck Airo, Lucy Mayenga, AnaMaryStella Mallac, Mchungaji Luckson Mwanjale, Mwanamrisho Abama, Diana Chilolo, Ignus Malocha, Saidi Bungara, Iddi Azzan, Neema Mgaya Hamid, Sara Msafiri, Dk. Engelbert Ndugulile na Maulidah Komu.
KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Edward Lowassa, Anastazia Wambura,
John Shibuda, Khalifa Suleiman Khalifa,
Muhammad Sanya, Leticia Nyerere, Thuwayba Idrisa Muhamed, Susan Lymo, Faith Mitambo, Juma Nkamia,Betty Machangu, Selemani Jafo, Mussa Azzan Zungu, Salim Hemed Khamis na Yussuf Hamad Masauni,
KAMATI YA BAJETI
Andrew Chenge, Christine Mughway Lissu, Kidawa Hamid Saleh, Mansoor Shaniff Hiran, Saada Mukya Salum, Amina Abdallah Amour, Joseph Selasini, Josephat Kandege, Dk. Cyril Chami, Dk. Fetus Limbu, Mwigulu Nchemba, Assumpter Mshama, James Mbatia, Beatrice Shellukindo na Hamad Rashid Mohamed.
KATIBA, SHERIA NA UTAWALA
Abas Zuberi Mtemvu, Tundu Lissu, Gosbert Blandes, Pindi Chana, Nimrod Mkono, Felix Mkosamali, Nyambari Nyangwine, Fakharia Khamis Shomari, Rukia Kassim Ahmed, Jaku Hashim Ayoub, Mustapha Akunaay, Ramadhan Haji Saleh, Jasson Rweikiza,
William Ngeleja, Deogratias Ntukamazina, Ali Khamis Seif, Mariam Kasembe, Abdallah Sharia Ameir na Halima Mdee.
KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA
Mahmoud Mgimwa, Habib Mnyaa, Margaret Mkanga,
Haji Khatib Kai, Ester Midimu, Hassein Nassor Amar, Ahmed Juma Ngwali, Luhaga Mpina, Dk. Titus Kamani,Joyce Mukya, David Kafulila, Shawana Bukhet Hassan,Said Mussa Zubeir, Vicky Kamata, Naomi Kaihula, Khatibu Said Haji, Freeman Mbowe, Amina Mwidau,
Josephine Genzabuke, Dunstun Kitandula na Mohamed Misanga.
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Anna Abdallah, Dk. Muhamed Seif Khatib, Kapteni John Chiligati, Augustino Masele, Masoud Abdallah Salim, Mussa Hassan Mussa, Omar Nundu, Stella Manyanya, Cynthia Ngoye, Henry Shekiffu, Vita Kawawa, David Mallole, Hamad Ali Hamad, Rachel Mashishanga, Dk. Augustino Mrema na Vincent Nyerere.
KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII
Fatuma Abdallah Mikidadi, Ritta Mlaki, Riziki Omari Juma, Salome Mwambu, Ali Juma Haji, Faki Haji Makame, Margareth Sitta, Ezekia Wenje, Agripina Buyogera, Juma Sururu Juma, Mchungaji Dk. Getrude Rwakatare, Abia Nyabakari, Zabein Mhita, Mohamed Dewji, Dk. Anton Mbasa, Steven Ngonyani, Martha Umbulla, Profesa Kulikoyela Kahigi, Asnain Murji, Cecilia Paresso na Abdulaziz Aboud.
MAENDELEO YA JAMII
John Komba, Moza Abedi Saidy, Joseph Mbilinyi,
Mohamed Said Mohammed, Nasib Suleiman Omar, Mustafa Mkulo, Jenista Mhagama, Salum Barwany, Kiumbwa Makame Mbaraka, Salvatory Machemuli, Livingstone Lusinde, Saidi Mtanda, Agness Hokororo, Godbless Lema, Mary Chatanda, Juma Othman Ali, Jaddy Simai Jaddy, Dk. Maua Daftar, Albert Obama,
Rose Kamili Sukum na Rosemary Kirigini.
KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI
David Homeli Mwakyusa, Dk. Christine Gabriel Ishengoma,
Asaa Othman Hamad, Abdulsalaam Selemani Ameir, Said Juma Nkumba, Abdllah Haji Ali, Haji Juma Sereweji, Lolensia Masele Bukwimba, Mch. Peter Simon Misigwa, Prof. Peter Mahmudu Msolla, Nameloki Edward Moringe Sokoine, Dk. Lucy Sawere Nkya,
Sylvestry Francis Koka, Kheri Khatib Ameir, Meshack Jeremia Opulukwa,Philemon Kiwelu Ndesamburo, Jitu Vrajlal Soni, Sadifa Juma Khamis, Donald Kelvin Max, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, Subira Khamis Mgalu na Magdalena Hamisi Sakaya,
KAMATI YA MIUNDOMBINU
Peter Joseph Serukamba, Maryam Salum Msabaha, Clara Diana Mwatuka, Zamda Shamte Madabida, Innocent Edward Kalogeris, Hussein Mussa Mzee, Aliko Nikusuma Kibona, Said Ramadhani Bwanamdogo, Zahra Ali Hamad, Ahmed Mabkhut Shabiby,Dk. Pudenciana Wilfred Kikwembe, Mussa Haji Kombo, Juma Athuman Kapuya, Mtutura Abdallah Mtutura, Abdul Rajab Mteketa, Suleiman Masoud Nchambi, Saidi Amour Arfi, Ramo Matala Makani, Rebecca Michael Mngodo na Elizabeth Nkunda Batenga.
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI
Deusiderius John Mipata, Deo Haule Filikunjombe,
Asha Mshimba Jecha, Lucy Phillemon Owenya,
Ester Nicholas Matiko, John Momose Cheyo, Zainab Matitu Vulu, Ally Keissy Mohamed, Zainab Rashid Kawawa, Kheri Ali Khamis, Faida Mohamed Bakari, Ismael Aden Rage, Modestus Dickon Kilufi, Abdul Jabir Marombwa, Gaudence Casssian Kayombo, Kombo Khamis Kombo na Catherine Valentine Magige.
KAMATI ZA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA
Tauhida Cassian Galosi Nyimbo, Dunstan Daniel Mkapa, Azza Hillal Hamad, Yahya Kassim Issa, Menrad Lutengano Kigola, Bahati Ali Abeid, Kulthum Jumanne Mchuchuli, Rajab Mbarouk Mohammed,Yusuph Abdallah Nassir, Philipa Geofrey Mturano, Eustas Osler Katagira, Muhonga Said Ruhwanywa, Munde Tambwe Abdallah, Ezekiel Magolyo Maige,Mch. Israel Yohana Natse, Alfaxard Kange Lugola, Felista Aloyce Bura na Suleiman Jumanne Zedi.
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
John Paul Lwanji,Hamis Andrea Kigwangalla,
Godfrey Weston Zambi, Highness Samson Kiwia, Benardetha Kasabago Mushashu, Asha Mohamed Omari, Dk. Kebwe Stephen Kebwe, Rosweeter Faustine Kasikila, Christopher Olonyokie Ole-Sendeka, Eugen Elishininga Mwaiposa, Rashid Ali Abdallah, Athuman Rashid Mfutakamba, Pauline Gekul,Sabreena Hamza Sungura, Mkiwa Adam Kimwanga, Mariam Salum Mfaki, Moses Joseph Machali na Sylvester Masele Mabumba.
KAMATI YA NISHATI NA MADINI
Victor Kilasile Mwambalaswa, Saleh Ahmed Pamba, Josephine Tabitha Chagulla David Ernest Silinde, Martha Moses Mlata, Devotha Mkuwa Likokola, Raya Ibrahim Khamis, Mariam Nassor Kisangi, Murtaza Ally Mangungu, Juma Abdallah Njwayo, Jerome Dismas Bwanausi, Richard Mganga Ndassa Anne Kilango Malecela , Charles John Paul Mwijage,Herbert James Mntangi, Shaffin Ahmedali Sumar, Yussuf Haji Khamis na Riziki Saidi Lulida.
KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
James Daud Lembeli, Abdulkarim Esmail Hassan Shah,
Sylvester Mhoja Kasulumbayi, Zakia Hamdani Meghji, Susan Limbweni Aloyce Kiwanga, Dk. Mary Machuche Mwanjelwa, Muhamad Amour Chomboh, Waride Bakar Jabu, Kaika Saning’o Telele, Amina Andrew Clement, Ester Amos Bulaya, John John Mnyika, Michael Lekule Laizer, Mwanakhamis Khasim Said, Salim Hemed Khamis, Al-Shymaa Kwegyr, Grace Sindato Kiwelu. Salim Abdullah Turky, Abuu Hamoud Juma na Kisyeri Werema Chambir

Comments
Post a Comment