STORI YA KANISA KUVAMIWA NA UAMSHO HII HAPA




na Danson Kaijage, Dodoma

.


WAUMINI wa Kanisa Kuu la Roma Jimbo la Dodoma wamevamiwa na mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni mwanachama wa kikundi cha Uamsho.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo, Arubert Bura ambaye alizungumza na Tanzania Daima Jumapili alisema jana majira ya saa 5:50 asubuhi kuna kijana alikuwa amevaa mavazi yanayotambulisha imani ya Kiislamu na kuingia lango kuu na kufika moja kwa moja altare na kuanza kusujudu na kuondoka.
Bura alisema baada ya kutokea tukio hilo Padri Baptist Mapunda alianza kukemea hali hiyo na muda mfupi waumini wa kanisa hilo walimtia nguvuni kijana huyo na kuanza kumhoji alikotokea na anakokwenda.
Kwa mujibu wa maelezo ya zee wa kanisa hilo walianza kumhoji kijana huyo ambapo alijitambulisha kwa jina la Hassan Saidi, na kudai kuwa amezaliwa mwaka 1987 huku vyeti vyake halisi vya kuzaliwa vinaonesha kazaliwa mwaka 1989.
Alisema katika begi la mtuhumiwa huyo alipopekuliwa alikutwa na leseni ya kuendeshea gari, vyeti halisi vya kuzaliwa pamoja na vivuli vyake, vyeti vya elimu ya shule ya msingi na sekondari.
Aidha, alisema baada ya kuendelea kupekua katika mkoba wake ambao ulikuwa kama wa kubebea kompyuta mpakato (Laptop) walibaini kuwa alikuwa na ubani, majarida pamoja na kitabu kimojawapo kilichokuwa na ramani ya mji wote wa Dar es Salaam iliyoonesha misikiti na makanisa.
Bura alisema baada ya kuendelea kumbana kijana huyo, alisema kuwa yeye ni dereva wa magari. Pia alikuwa na cheti cha mafunzo ya udereva cha VETA, pamoja na vyeti vya matibabu.
Mzee huyo wa kanisa alisema katika kuendelea kupekuwa walibaini cheti cha kuchukulia dawa katika Hospitali ya Milembe ambayo iko nje kidogo ya mji.
Kwa mujibu wa maelezo ya Bura kutokana na hofu ya tukio hilo, walilazimika kumpeleka katika kituo cha polisi ambako yeye na mtuhumiwa huyo waliandika maelezo.
Kamanda Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa ofisini kwake hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa nje kwa muda huo.
Baadaye alipopigiwa simu iliita bila kupokelewa, akatumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms), ambapo baada ya muda alipiga simu.
Alipoulizwa tukio hilo alisema hana taarifa nalo na kuomba aelezewe tukio hilo na mwandishi wa habari.
Alipoelezwa alionesha kutolifahamu japo baadaye alisema kuwa taarifa alizonazo si za mtu wa jinsi hiyo.
“Hapana mimi siamini kama mtu huyo atakuwa ni wa kikundi cha Uamsho, nahisi atakuwa na mambo mengine. Lakini kwa jambo hilo mimi sina taarifa hizo, kama mnataka kuandika andika, lakini mimi sijui,” alisema Kamanda Misime.

Comments

Popular Posts