STORI YA MWANAFUNZI WA IFM ALIYRKUTWA AMEKUFA HOSTEL
Chuo cha IFM
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio
hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D
kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
Jamiileotz lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi,
Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya
Usimamizi wa Kodi akiwa mwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda
kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala na wanafunzi kutoka nje ya
nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili ya masomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa
wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuo hiki, kwa hapa
chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika
katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa
umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi
na polisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi
Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce,
aliliambia jamiileotz kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo
chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea
hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi
tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika Machava Hostel ndiko
anakolala,” alisema Alphonce.
Comments
Post a Comment