TAZAMA PICHA HIZI JINSI RAIS KIKWETE ALIVYOSHIRIKI MSIBA WA YANGA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Lawrence
Mwalusako katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha
wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika
makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. wengine toka kushoto ni Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Ndugu Adam Malima, Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es salaam Mhe Ranmadhani Madabida na kulia ni
Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji
.
Rais
Jakaya Kikwete akiondoka baada ya kuongoza maelfu ya waombolezaji
katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan
Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya
Kisutu jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA IKULU).
Athuman Kilambo ambaye alifariki dunia usiku za kuamkia leo baada ya kusumbuliwa kwa muda na ugonjwa wa kansa amezikwa kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Kilambo alikuwa mlinzi hodari wa kushoto wa timu ya Yanga ambayo aliichezea kwenye miaka ya 1960 na 1970. Alikuwa mmoja wa walinzi imara wa kikosi cha klabu hiyo ambacho kilitawala soka ya Tanzania kwa kushinda ubingwa nchini kwa miaka mitano mfululizo hadi mwaka 1973 wakati Simba ilipowavua ubingwa huo.

Comments
Post a Comment