Vyombo vya habari Somalia vyafanya kampeni kuachiwa huru kwa mwandishi wa habari aliyefungwa
Vyombo vya Habari vya Somalia vilitangaza Jumatatu (tarehe 4 Machi) kuzinduliwa kwa kampeni dhidi ya kufungwa kwa mwandishi wa habari Abdiasis Abdinuur Ibrahim kwa miezi sita kwa kumhoji mtuhumiwa aliyedaiwa kubakwa.
Wawakilishi kutoka katika magazeti, redio, televisheni na vyombo vya habari vya mtandaoni walikusanyika huko Mogadishu kutoa tamko la pamoja dhidi ya hukumu ya Ibrahim katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Waandishi wa Habari wa Somalia (NUSOJ) na kufadhiliwa na Wanaharakati wasiokuwa Serikalini Kusini mwa Somalia ya Kati, Redio RBC ya Somalia iliripoti.
"Tumekubaliana kuunganisha nguvu na kuandika barua kwa Rais, waziri mkuu na spika ikielezea kero zetu na kutaka kuachiwa kwa mwenzetu, ambayo itasainiwa na waajiriwa wa vyombo vya habari pamoja na NUSOJ," alisema katibu Mkuu wa NUSOJ Mohamed Ibrahim. "Pia tumekubaliana kuzindua taarifa za matukio ya kina ya siku, kampeni ya vyombo vya habari inayolenga kwenye kuachiwa kwa mwandishi wa habari, hukumu, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza."
Mwezi uliopita, Ibrahim alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuzikosea taasisi za serikali, lakini adhabu hiyo ilipunguzwa kuwa miezi sita na mahakama ya rufaa Jumapili

Comments
Post a Comment