Wafanyabiashara Moshi watishia kuiburuza Manispaa mahakamani
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
Wakizungumza na Mwandishi wa blogu hii, Makamu Mwenyekiti wa wenye vibanda kwenye soko hilo, Gerald Mrutu, alisema kwa sasa wanatozwa kodi ya pango ya Sh. 180,000, huku kukiwa na makubaliano baina yao na Manispaa kwenye ujenzi wa vibanda hivyo.
Alisema mwaka 1999, Manispaa ilitafuta watu kwa ajili ya kuwekeza kwa kujenga uzio kuzunguka soko hilo na walipewa hati miliki ya miaka 33 na wafanyabiashara 89 walijitokeza na kugawiwa maeneo.
“Tulipewa ardhi na Wizara ya Ardhi, na idhini ya kujenga kwa gharama zetu wenyewe, sisi ni wamiliki na si wapangaji kama Manispaa inavyosema kwa sasa,” alisema.
Alisema walianza kulipa ada ya ardhi ya Sh. 750 mwaka 1992 ilifika 5,000, 1997 Sh 6,000, 2002 Sh 30,000, 2007 360,000, kukiwa na ongezeko kubwa na ushirikishwaji duni miongoni mwao, huku sheria ikitaka kubadilika kwa bei hizo kila baada ya miaka mitano.
Mrutu alisema walimfuata Mkurugenzi na kuzungumza naye kupinga ongezeko hilo ambalo halifuati utaratibu wa kisheria na akashusha hadi Sh. 180,000 ambayo ililetwa ikiwa na sheria ndogo.
Alisema kodi hiyo ni kandamizi kwa kuwa wapo wafanyabiashara wengine wanaomiliki eneo la mita za mraba 75 karibu na eneo hilo, hulipa Sh. 75,000 kwa mwaka.
“Tumeomba kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa na wataalam wengine, kwenye meza ya mazungumzo lakini tunapigwa danadana, tumemwandikia Mkuu wa Mkoa akaagiza tukutane, tukatuma maswali 13 hayajajibiwa hadi sasa…kwa sasa tunadhamiria kwenda mahakamani,” alisema

Comments
Post a Comment