WALINZI WA MKE WA RAIS MUSEVENI KUTIMULIWA BUNGENI
|
Walinzi wawili wa mke wa Rais
wa Uganda Mama Museveni, walitolewa nje ya ukumbi wa bunge la nchi hiyo
baada ya kuingia wakionekana wamebeba bastola ambazo waziwazi wengi
waliziona. Kilichofanya watolewe ni malalamiko ya Wabunge kadhaa akiwemo Joseph Sewungu ambae alieleza kuogopa baada ya kuziona hizo bastola huku wengine baadhi wakisema hawajioni kama wako salama. Mbunge wa Mbale Jack Wamayi aliuliza kulikoni mpaka walinzi hao wa mama kuruhusiwa kuingia na bastola wakati walinzi wa baba ambae ndio Rais hawajawahi kufanya kitendo kama hicho. |

Comments
Post a Comment