Wateja walalamikia usumbufu wa kununua luku kwa simu

Meneja wa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud
Baadhi ya wateja wa huduma ya luku, wameyalalamikia makampuni ya simu kwa kile walichoeleza ni usumbufu kwenye manunuzi ya umeme wa luku.

Baadhi ya wateja hao Neema Mgaya na Mary Mayalla, walisema huduma hiyo imekuwa na usumbufu mwingi.

“Nimenunua umeme kwa siku tatu fedha zangu zimekatwa lakini sijapata umeme, nimefuatilia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wanasema nifuatilie kwenye kampuni ya simu,” alisema.

Alisema huduma hiyo imekuwa yenye usumbufu mkubwa kwa wateja kwani uhakika wa kupata umeme alionunua kwa haraka ni mdogo na wakati mwingine asipate kabisa na fedha imekatwa.

Meneja wa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema tatizo hilo halipo kwenye shirika hilo bali kwa kampuni ya simu ambayo mteja ametumia na kuwataka wateja kwenda kwenye ofisi za kampuni husika kupata ufafanuzi.

Naye Msemaji wa kampuni ya Vodacom, ambayo baadhi ya wateja wameilalamikia, Martine Nkurlu, alisema teknolojia mpya ina mapungufu yake na jinsi wateja wanavyoitumia.

Alisema wateja waliokubwa na tatizo hilo, wanatakiwa kwenda kwenye ofisi za kampuni hiyo kwa msaada zaidi, kwani wengine hukosea jinsi ya kutumia na kujikuta fedha zilipoelekezwa kwenda siyo sehemu husika.

Comments

Popular Posts