Wavamizi wawaua 25 nchini Nigeria
Takriban watu 25 wameuawa
wakati watu waliojihami kwa bunduki walipovamia jela, kituo cha polisi,
benki na baa katika mji wa Ganye, mashariki wa Nigeria, polisi wamesema.
Mashambulizi hayo, yaliyofanywa kwa pamoja, yalitokea Ijumaa, lakini maafa yalijulikana tu Jumamosi.Hakuna kundi lolote ambalo limesema ndilo lililofanya mashambulizi hayo, ingawaje polisi wanadhani kwamba yawezekana kuwa ni wapiganaji wa kundi la Kiisilamu la Boko Haram
.
Wavamizi hao – waliokuwa na mabomu, bunduki za rashasha na guruneti zinzofyatuliwa na roketi – waliwafungulia jela mahabusu kadhaa, duru rasmi zilisema.
Watu saba walipigwa risasi na kuuwawa ndani ya baa, sita karibu na benki, na wengine wakiwa nje ya nyumba zao na mtaani.
Haijulikani ni kiasi gani cha pesa zilizoibwa.
Boko Haram yasema kwamba kusudi lake ni kupigana ili kuunda serikali ya Kiisilamu Nigeria kaskazini.
Yaaminika kwamba kikundi hicho pia kina wanachama nchini Cameroon, Niger na Chad.
Comments
Post a Comment