WAZIRI MAGUFULI AKIPIGA NGOMA NDANI YA MSONDO NGOMA BENDI
Waziri
wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya
Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani
Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Kushoto ni wanamuziki wa bendi hiyo,
wakimshabikia.
Wanamuziki
wa bendi ya Msondo Ngoma, wakionyesha umahiri wao wa kupuliza 'midomo
ya bata' wakati wa bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara
jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma
Comments
Post a Comment