WEMA SEPETU AFANYA KUFURU YA PESA TENA:ATUMIA MIL 6.5 KUWAFANYIA MBWA WAKE SHOPPING.




Staa wa bongo movie na mmilikiwa kampuni ya Endless love film anayejulikana kama Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amefanya kufuru kwa mbwa wake wawili baada ya ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya TSh. milioni 6.5)




Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.
Baada ya yeye kuulizwa alikuwa na haya ya kusema
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”



Mbwa hao wa Wema Sepetu aliowapa majina ya Van na Gucc wamekuwa ni gumzo kutokana na jinsi anavyowahudumia huku akiajiri watu maalumu wa kuhakikisha wanavaa, kula na kulala pazuri.

Comments