Wengi wajitokeza kutoa maoni kwa Tume ya Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Wananchi wengi wamejitokeza kutoa maoni yao, kwenye Tume  ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome, aliiambia Jamiileotz jana kuwa wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika kila shule ambazo tume imetembelea baada ya kupata taarifa za uwapo wa wajumbe wa tume ili na wao wapate fursa ya kutoa maoni yao
.

Profesa Mchome alisema jambo hilo linatia moyo na linaonyesha kuwa tume hiyo itapata ushirikiano wa kutosha katika kila eneo ambalo wajumbe wake watapita ili kukusanya maoni kwa muda waliopewa.

“Kila wanapopata taarifa ya kuwapo kwa wajumbe wetu, na kuna maeneo ambayo idadi ya wananchi imekuwa ni kubwa sana, lakini wote tumewapa nafasi ya kutoa maoni yao,” alisema Profesa Mchome

Aliongeza kuwa tume yake imejigawa katika maeneo tofauti katika mkoa wa Dar es Salaam na kwamba  kwa sasa inaendelea kuwahoji wanafunzi pamoja na walimu, wakuu wa shule, bodi za shule, wazazi na wananchi kwa ujumla.

Tume hiyo wiki ijayo inatarajia kwenda Kanda ya Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Masharik

Comments

Popular Posts