AIBU: MBUNGE MSTAAFU AFUMANIWA NA MKE WA MFANYAKAZI WAKE;SOMA STORI KAMILI IKO HAPA
Mtego wa kumnasa ulifanikiwa baada ya
mtuhumiwa kutinga hotelini hapo akiwa na gari la kampuni aina ya Toyota
Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY na kunyooka moja kwa moja
chumbani alikokuwa akisubiriwa na mwanamke huyo.
Habari za uhakika zilieleza kuwa bosi huyo ni mbunge mstaafu aliyewahi
kuwa Mheshimiwa wa Jimbo la Nkotakota South East nchini Malawi kwa
kipindi cha miaka kadhaa.
Jamaa huyo aliangushwa na Agness Chatipwa Mandebvu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 nchini humo ndipo akatinga jijini hapa na kupata kazi ya umeneja wa kampuni hiyo ya usafirishaji. Ilidaiwa kuwa meneja huyo ndiyo mchezo wake kwa sababu amekuwa akiwafanyia hivyo mabinti wanaofika ofisini kwake kwa ajili ya kuomba kazi ambapo huwakubalia kuwapa kazi endapo watakubali kushiriki naye dhambi ya uzinzi. Uchunguzi ndani ya kampuni hiyo ulidaka madai kuwa tangu awe meneja, mabinti zaidi ya watano waliacha au kufukuzwa kazi walipokataa kufanya naye ngono. Ilidaiwa kuwa wanaokubaliana na hali hiyo kutokana na ugumu wa maisha humkubalia na kupandishwa vyeo kiholela. Sakata la tabia hiyo chafu kwa raia wa Kitanzania, lilifikia kikomo baada ya mfanyakazi mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa meneja huyo kusimamishwa kazi kwa madai kuwa alichelewa kuripoti kazini. Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwa bosi wake, alisimamishwa kazi ambapo bosi huyo alitumia mwanya huo kuanza kumchombeza mke wa jamaa huyo kwa kumwambia amkubalie ili amrudishe mumewe kazini. Baada ya kupata usumbufu huo kwa kipindi kirefu ndipo jamaa huyo pamoja na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa hawaipendi tabia ya bosi wao wakaandaa mtego uliomnasa kama panya bila kujinasua na kuishia mikononi mwa polisi. Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo ambao majina yake hawakutaka yaandikwe , walisema tabia ya bosi wao imekithiri na kwamba amekuwa akitumia wadhifa wake kuwalaghai watoto wa kike ili kufanya nao mapenzi. Wafanyakazi hao walidai ni bora Idara ya Uhamiaji mkoani hapa iingilie kati suala hilo ili kuwanusuru Watanzania dhidi ya watumishi wa kigeni wanaokuwa na tabia zinazolenga kuwaondolea utu wao. Baada ya kufumaniwa akiwa mtupu kutokana na mke wa mtu huyo kutoa ishara kwa walioweka mtego, aliomba radhi kwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni mwajiriwa wa kampuni anayefanya kazi ya kutengeneza bustani. Hata hivyo, msamaha wake ulikataliwa na soo likatinga polisi na sasa anasubiriwa kupelekwa mbele ya mkono wa sheria... |
Comments
Post a Comment