AL-SHABABU KWA MTNDO HUU LAZIMA WAPATIKANE
Askari wa Jeshi la Polisi, akimpekua padri kwenye
eneo la kuingilia Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam
wakati wa ibada ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka juzi. Ulinzi uliimarishwa
katika kanisa hilo kwa kumpekua kila aliyekuwa akiingia. Hatua hiyo
inatokana na mfululizo wa matukio ya vitisho na mashambulizi dhidi ya
viongozi wa dini nchini.
Ukaguzi huo ulifanyika kwenye lango la geti kuu kabla ya kuingia
ndani ya kanisa hilo kwa ibada ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka ukihusisha
Waumini, Watawa, Mapadri, Askofu na watumishi wengine wa kanisa kabla
ya kuanza kwa ibada.
Walinzi wa kampuni binafsi walionekana wakiendelea na kazi hiyo
kuhakikisha kila anayeingia kanisani humo haingii na silaha yoyote
ambayo ni tishio kwa usalama wa kanisa na waumini wake.
Hatua hiyo imekuja kukiwa tayari kumetokea matukio ya kuchomwa moto
makanisa, kuibwa mali za kanisa, na hujuma nyinginezo kwa makanisa
maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam na kushambuliwa na kuuwawa kwa
viongozi wa kanisa.
Wakizungumzia hatua hiyo, baadhi ya waumini, Neema John na Joseph
Mwaipopo, walisema kwa kiasi fulani inashangaza lakini kwa kujiridhisha
kwenye suala la ulinzi ni vyema likawa zoezi endelevu hasa ikizingatiwa
hali tete iliyopo dhidi ya makanisa.
"Hatukuwahi kufikiri wakristo tutafikia hatua hii ya kutoaminina,
tuliabudu kwa wazi bila hofu yoyote, kwa imani za dini zetu Watanzania
tunapaswa kumuomba Mungu lulu ya amani tulioyonayo isitoweke," alisema
Mwaipopo.
Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Polcarp Kadinali
Pengo, aliwataka waumini waliobatizwa kwa siku hiyo na wengine
kusisimama kwenye imani yao kuwa mfano mzuri kwa wanajamii wengine.

Comments
Post a Comment