Skip to main content
BALOTELLI AENDELEZA VITUKO VYAKE ITALIA
.
NYOTA wa zamani wa klabu
ya Manchester City mwenye vituko vingi, Mario Balotelli ameonyesha
kushindwa kupigwa picha akiwa amelala katika sehemu ya kuwekea mizigo
katika treni walioyokuwa wakisafiri nayo. Katika
picha hiyo Balotelli alionekana akiwa na nyota wenzake wa klabu yake ya
AC Milan M’Baye Niang na Stephan El Shaarawy wote wakiwa wameacha viti
vilivyopo katika treni hiyo na kukwea juu kwenye mizigo. Balotelli
alihamia Milan Januari baada ya kucheza katika klabu ya Manchester City
kwa misimu miwili na nusu na toka arejee nyumbani kwao amekuwa akicheza
kwa kiwango cha juu baada ya kufunga mabao matano katika mechi sita za
Serie A. Nyota
huyo pia alifunga mabao yote ya timu yake ya taifa ya Italia iliyoshinda
mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe ya Dunia dhidi ya
Malta wiki iliyopita
Comments
Post a Comment